Manchester, England
Beki wa zamani wa Man City, Benjamin Mendy (pichani) amefutiwa tena tuhuma nyingine za kumbaka msichana wa miaka 24 na kutaka kumbaka msichana mwingine wa miaka 29.
Mendy mwenye umri wa miaka 28 ambaye pia ni beki wa timu ya Taifa ya Ufaransa alidaiwa kufanya makosa hayo Oktoba 2020 katika mjengo wake wa kifahari na kujikuta akiondolewa katika kikosi cha Man City.
Uamuzi huo wa mahakama ya Chester Crown uliofikiwa jana Ijumaa ni nyingine kubwa kwa mchezaji huyo ambaye Januari mwaka huu alifutiwa makosa mengine sita ya tuhuma za kubaka na udhalilishaji kijinsia.
Baada ya mahakama kumfutia makosa hayo katika shauri lililoendeshwa kwa kipindi cha wiki tatu, Mendy alijikuta akimwaga chozi.
Majaji sita wanaume na sita wanawake walifikia uamuzi huo baada ya mashauriano ya takriban saa tatu kabla ya kutangaza kumfutia mchezaji huyo tuhuma zilizokuwa zikimkabili.
Mendy ambaye amekuwa akiandamwa na tuhuma hizo kwa takriban miaka miwili sasa, mkataba wake na Man City ulifikia ukomo mapema mwezi huu.
Katika mshtaka ya awali Mendy alikuwa na tuhuma za makosa sita ya kubaka na moja la udhalilishaji kijinsia ambayo alidaiwa kuwafanyia wasichana wanne.
Wakati kesi hiyo ikiendelea muendesha mashtaka mmoja aliiambia mahakama kwamba Mendy alikuwa na tabia ya kufanya sherehe za kifahari nyumbani kwake na kutumia nafasi hiyo kuwanasa wageni wasichana akitumia utajiri na umaarufu wake uliomfanya awe mtu asiyekubali kuambiwa hapana.
Mahusiano Mendy afutiwa kesi ya ubakaji
Mendy afutiwa kesi ya ubakaji
Read also
