Na mwandishi wetu
Klabu ya Medeama ya Ghana imemfuta kazi kocha wake mkuu, Evans Adotey (pichani) baada ya kipigo cha juzi Jumatano cha mabao 3-0 kutoka kwa Yanga kwenye mchezo wa makundi wa Ligi ya Mabingwa Afrika.
Kocha huyo amevuliwa wadhifa huo na sasa amerejeshwa kwenye cheo chake cha awali cha ukurugenzi wa ufundi wa timu hiyo.
Adotey ameiongoza timu hiyo katika mechi nne za makundi za Ligi ya Mabingwa na kuvuna alama nne na kushika nafasi ya mwisho kwenye Kundi D, kinara wake akiwa ni Al Ahly yenye pointi tano baada ya mechi tatu.
Yanga baada ya ushindi dhidi ya Medeama kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam, sasa inashika nafasi ya pili kwa pointi tano pia baada ya mechi nne huku ya tatu ni CR Belouizdad iliyocheza mechi tatu na kukusanya pointi nne.
Kwenye Ligi Kuu Ghana, Adotey ameiongoza timu hiyo katika michezo 11, ikiambulia pointi 16, ikishika nafasi ya 12 kwenye msimamo wa ligi hiyo yenye timu 18, imeshinda mechi tano, sare moja na kufungwa mara tano.
Kimataifa Kocha Medeama afutwa kazi
Kocha Medeama afutwa kazi
Read also