Manchester, England
Winga wa Manchester United, Cristiano Ronaldo amerudi katika mazoezi ya kikosi cha kwanza cha timu hiyo na huenda keshokutwa Alhamisi akacheza mechi ya Europa Ligi dhidi ya FC Sheriff.
Ronaldo aliondolewa katika kikosi hicho na kocha Eric ten Hag na akakosekana Jumamosi iliyopita katika mechi dhidi ya Chelsea iliyoisha kwa sare ya bao 1-1. Ten Hag alimuondoka katika kikosi chake baada ya mchezaji huyo kususa kuingia uwanjani na baadaye kuondoka kabisa dakika chache kabla ya mpira kumalizika katika mechi na Tottenham iliyoisha kwa Man United kutoka na ushindi wa 2-0.
Katika uamuzi huo, Ten Hag alimtaka mchezaji huyo Ijumaa afanye mazoezi ya peke yake na makocha wasaidizi na jana Jumatatu wachezaji wa kikosi cha kwanza walipewa muda wa kupumzika lakini leo Jumanne wameanza mazoezi ya pamoja na Ronaldo ameruhusiwa kuungana nao kwa ajili ya mechi ya keshokutwa Alhamisi dhidi ya FC Sheriff.
Habari za ndani zinadai kuwa hata Ten Hag kwa sasa anafuraha baada ya utata kati yake na mchezaji huyo kumalizwa ambapo kocha huyo na mchezaji wake kwa pamoja wapo tayari kuangalia yajayo.
Ten Hag licha ya kuwa na ugomvi na mchezaji huyo na kukiri kwamba anatakiwa kuadhibiwa lakini Ijumaa iliyopita alinukuliwa akisema kwamba Ronaldo anabaki kuwa mmoja wa wachezaji muhimu kwenye kikosi chake.
“Tulichosema katika taarifa yetu ni kwamba Cristiano anabaki kuwa mmoja wa watu muhimu katika kikosi na tunamtegemea kwa ajili ya kipindi chote cha msimu, tunataka kukamilisha malengo yetu, nataka awemo kwenye kikosi na kuhusika katika kila mechi kwa sababu ana msaada,” alisema.
Ronaldo hadi sasa amefunga mabao mawili katika mechi 12 tangu kuanza kwa msimu huu, hapo hapo anajivunia kufunga bao lake la 700 alilolipata katika ushindi wa mabao 2-1 ambao timu hiyo iliupata katika mechi yake na Everton.
Kimataifa Ronaldo arudi kikosini Man Utd
Ronaldo arudi kikosini Man Utd
Green SportsAuthor / Greensports Media LTD
Greensports author
Read also
