London, England
Ratiba ya Ligi Kuu England msimu wa 2022/23 imetangazwa rasmi ikionyesha kuwa ligi hiyo itaanza kutimua vumbi Agosti 5 mwaka huu kwa mabingwa watetezi, Man City kuanza kulitetea taji hilo ugenini dhidi ya West Ham.
Kwa ajili ya fainali za Kombe la Dunia, ligi hiyo italazimika kusimama mwezi Novemba kupisha fainali hizo baada ya agizo la Fifa kutaka wachezaji waruhusiwe kujiunga na timu zao za Taifa kuanzia Novemba 14.
Safari hii ligi hiyo imeanza mapema, siku 75 baada ya msimu wa 2021/22 kumalizika na itamalizika kwa kuchelewa kutokana na kuingiliana na fainali za Kombe la Dunia ambazo kwa kawaida hufanyika mwezi Juni na Julai lakini safari hii fainali hizo zinafanyika Qatar kati ya Novemba na Desemba, hiyo maana yake ni kwamba mapumziko ya msimu safari hii itakuwa ni wiki sita na siku kadhaa.
Mechi ya Man City na West Ham inakumbusha mechi ya mwisho baina ya timu hizo zilipokutana msimu uliopita na Man City kulazimika kusawazisha mabao mawili waliyofungwa na hatimaye kumaliza mchezo huo kwa sare ya 2-2.
Ukiachana na mechi hiyo ambayo itachezwa Agosti 7 yaani Jumapili, Agosti 5 (Ijumaa) siku ambayo pazia la ligi hiyo litafunguliwa rasmi kutakuwa na mechi moja ambapo Arsenal watakuwa wageni wa Crystal Palace. Mechi za kufungua msimu kwa timu zote ni kama ifuatavyo…
Ijumaa, Agosti 5, 2022
Crystal Palace v Arsenal
Jumamosi Agosti 6, 2022
Fulham v Liverpool
Bournemouth v Aston Villa
Leeds United v Wolverhampton
Leicester City v Brentford
Newcastle United v Nottingham Forest
Tottenham Hotspur v Southampton
Everton v Chelsea
Jumapili, Agosti 7, 2022
Man United v Brighton
West Ham v Man City
