Na mwandishi wetu
Hatimaye yametimia baada ya Simba kumtambulisha rasmi kwenye kikosi chao kiungo Nassor Kapama kutoka Kagera Sugar, ikiendelea kujiweka sawa kuelekea msimu mpya wa 2022-23.
Usajili wa Kapama katika klabu ya Simba ni miongoni mwa sajili zilizokuwa zikitajwa kwa muda mrefu kiasi cha kusubiriwa siku na saa ya kuwekwa wazi kwa dili hilo linalotajwa kuwa la kandarasi ya miaka miwili.
Kapama ambaye amekuwa na kiwango bora kwenye msimu uliopita pia uwezo wake wa kumudu kwa ufasaha nafasi za mshambuliaji, kiungo na beki ni kitu kingine kilichowavutia mabosi wa Wekundu hao ambao wanapambana kusuka kikosi cha ushindani mkubwa zaidi msimu ujao baada ya msimu uliopita uangukia pua.
Simba katika kuonesha namna gani wanajivunia uwezo wa mchezaji huyo, walimtambulisha kwa maneno machache kwenye ukurasa wao wa mtandao wa kijamii wa Instagram: “Kipaji kikubwa kutoka kwenye ardhi iliyobarikiwa ya Tanzania kuja kuongeza nguvu kwenye kikosi chetu. Kapama ni Mnyama.”
Usajili wa Kapama ni wa pili kwa wachezaji wazawa ndani ya Simba baada ya utambulisho wa Habib Kyombo ambaye awali alisajiliwa na Singida Big Stars kutoka Mbeya Kwanza kabla ya kutangaza kuvunja mkataba wake kutokana na makubaliano yao, mchezaji na klabu atakayoenda.
Wachezaji wengine iliowatambulisha Simba mpaka sasa ni mshambuliaji Mzambia Moses Phiri kutoka Zanaco na kiungo Mnigeria, Victor Akpan aliyetua kutoka Coastal Union ya Tanga.
Soka Kapama atambulishwa Simba
Kapama atambulishwa Simba
Green SportsAuthor / Greensports Media LTD
Greensports author
Read also
