Na mwandishi wetu
Kuelekea mechi yao ya kesho ya Ligi Kuu NBC dhidi ya Namungo, Azam imeleeza kuwa imejiandaa vya kutosha kuhakikisha inaibuka na ushindi ili kutimiza ndoto yao ya kumaliza ligi ndani ya tatu bora.
Kocha Msaidizi wa Azam, Aggrey Morris alisema watahakikisha wanapata matokeo kwenye mechi hiyo itakayopigwa kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam ingawa wanafahamu hiyo ni mechi ngumu kwao kutokana na uzuri wa kikosi cha Namungo.
“Maandalizi yemakamilika, tumewapa wachezaji maelekezo jinsi ya kucheza kutokana na mpinzani alivyo. Lengo ni kushinda mechi kutokana na msimamo wa ligi ulivyo, tunataka ushindi ili kujihakikishia kumaliza nafasi ya tatu, tutakwenda kupambana kupata ushindi,” alisema Aggrey.
Naye kocha wa makipa wa Namungo, Faroukh Ramadhani alisema: “Tumekuja kupambana na Azam, shida yetu ni ushindi na furaha ili tumalize kwenye nafasi ya tano. Tunataka kumaliza kwenye nafasi ya tano, tunahitaji ushindi kuanzia mechi hii na Azam ili tulifanikishe hilo.”
Timu hizo zinakutana, Azam ikiwa imetoka kuifumua Ruvu Shooting mabao 3-1 huku Namungo nayo ikitaka kuendeleza matokeo bora kwenye mechi hizi za mwisho kama ilivyofanya kwenye mechi yake iliyipita kwa kuilazimisha Simba sare ya bao 1-1.
Azam ipo nafasi ya tatu kwa pointi 53 ikihitaji ushindi kuikimbia Singida Big Stars iliyo nafasi ya nne kwa pointi 51, Namungo wapo nafasi ya sita kwa pointi 36 wakiifukuzia Geita Gold iliyo juu yao kwa pointi 37.
Mechi nyingine mbili zitazikutanisha Coastal Union dhidi ya Ihefu na Kagera Sugar itapepetana na Tanzania Prisons.
Soka Azam yajipanga kuiadhibu Namungo
Azam yajipanga kuiadhibu Namungo
Read also
