Na mwandishi wetu
Mabondia sita wa Tanzania wanatarajia kuondoka nchini kesho Ijumaa kwenda Dakar, Senegal kushiriki mashindano ya kusaka tiketi ya kufuzu kwa Michezo ya Olimpiki ya Paris mwaka 2024.
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Ndondi Tanzania (BFT), Makore Mashaga (pichani) alisema leo Alhamisi kuwa Tanzania itawakilishwa na mabondia sita, wanaume wanne, wanawake wawili katika mashindano hayo yatakayoanza keshokutwa Jumamosi hadi Septemba 16, mwaka huu.
Makore aliwataja mabondia hao kuwa ni Yusuph Changarawe, Musa Malegesi, Mwalami Salum na Abdallah Mohamed wakati wanawake ni Zulfa Macho na Grace Mwakamele.
Msafara huo utakuwa chini ya Rais wa BFT, Lukelo Wilillo na viongozi wengine ambao ni Mashaga (kocha msaidizi), Samuel Kapunga (kcha mkuu) na Aisha George (matroni).
Mashaga alisema kwamba anaishukuru Serikali kwa kufanikisha safari hiyo baada ya kuwagharamia tiketi pamoja na posho wakati gharama za malazi na chakula watagharamia na waandaaji wa mashindano hayo.
Ngumi Mabondia wa Tanzania kwenda Dakar
Mabondia wa Tanzania kwenda Dakar
Read also
