Msanii aliyetambuliwa na ngoma ya Afrowave ‘Drogba’, Afro B, ameachia video yake mpya ya kibao ‘Wo Wo Wo’ ikiwa ni kolabo na Mmarekani, Rich The Kid na msanii wa muziki wa rap nchini Uingereza, Rimzee.
Afro B (pichani) ni raia wa Ivory Coast ambaye kwa sasa makazi yake yapo nchini Uingereza katika Jiji la London ametoa kolabo hiyo yenye hadhi ya kimataifa kwa kuwa inajumuisha mastaa kutoka mabara tofauti ulimwenguni.
Kabla ya kibao hiki, msanii huyo amepata kufanya kazi na mastaa wengine wa muziki wakiwemo, Wizkid, Slim Jxmmi (Rae Sremmurd), DJ Snake, Sukihana na wengineo.
Tangu wakati huo, amepata kuungwa mkono na Billboard, BET, BBC Radio 1, Capital, Hot 97, Power 105 na The Fader, Rolling Stone & NME.
“Mambo makubwa yanakuja, huu ni mwanzo tu, mashabiki wangu wakae mkao wa kula,” anasema Afro B akizungumzia kazi yake hiyo mpya.
Burudani Afro B aachia video ya Wo wo wo
Afro B aachia video ya Wo wo wo
Related posts
Read also