Na mwandishi wetu
Bao la dakika ya 89 lililofungwa na Habib Kyombo limeiwezesha Simba kutoka sare ya mabao 2-2 na KMC katika mechi ya Ligi Kuu ya NBC iliyochezwa leo kwenye Uwanja wa Benjamn Mkapa, Dar e Salaam.
Katika mechi hiyo, Simba ndio waliokuwa wa kwanza kupata bao katika dakika ya tatu ya mchezo huo mfungaji akiwa ni Moses Phiri, bao ambalo lilidumu kwa dakika 45 za kwanza kabla KMC hawajasawazisha dakika tatu baada ya kuanza kipindi cha pili mfungaji akiwa Matheo Antony.
Kabla Simba hawajatulia walijikuta wakipachikwa bao la pili dakika tisa baadaye mfungaji akiwa George Makang’a bao ambalo lilianza kuibua matumaini kwa KMC kutoka uwanjani na pointi zote tatu kabla Kyombo hajabadili matokeo
Sare ya Simba ni matokeo mengine yasiyopendeza kwa timu hiyo kama ilivyokuwa kwa mahasimu wao Yanga ambao jana nao waliambulia sare ya mabao 2-2 mbele ya Azam katika mechi iliyokuwa na ushindani mkali.
Katika mechi nyingine ya ligi hiyo, Mtibwa iliichapa Ihefu mabao 3-1 huku mabao ya washindi yakifungwa na Ismail Mhesa aliyefunga mawili katika dakika za 44 na 50 na Nickson Kibabage aliyefunga bao la tatu katika dakika ya 82 wakati bao pekee la Ihefu lilifungwa na Andrew Simchimba dakika ya nane ya mchezo huo.
Ligi hiyo itaendelea kesho kwa mechi kati ya Prisons na Mbeya City.
Soka Bao la Kyombo laiokoa Simba kuzama
Bao la Kyombo laiokoa Simba kuzama
Green SportsAuthor / Greensports Media LTD
Greensports author
Read also
