Na mwandishi wetu
Timu ya Geita Gold kesho inatarajia kufanya maandalizi yake ya mwisho kuwavaa wapinzani wao, Hilal Alsahil ya Sudan ambao walitarajia kuingia nchini leo jioni tayari kwa mechi ya marudiano ya Kombe la Shirikisho Afrika itakayopigwa kesho.
Geita ambayo inapambana kupindua matokeo ya kufungwa bao 1-0 na wapinzani wao hao wikiendi iliyopita walipokuwa ugenini, leo watafanya mazoezi ya mwisho kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam, uwanja ambao utatumika kwa ajili ya mchezo huo.
Akizungumza na GreenSports, Ofisa Habari wa Geita, Hemed Kivuyo alisema maandalizi yote kiujumla yamekwenda sawa na hata mshambuliaji wao hatari, George Mpole ambaye walimkosa kwenye mechi iliyopita, anaendelea na mazoezi kamili kwa ajili ya mtanange huo wa hatua ya awali.
“Kuhusu kikosi kipo vizuri na benchi la ufundi linaendelea na maandalizi yake ya mwisho ambapo kesho tutafanya mazoezi yetu ya mwisho pale Chamazi (Azam Complex) na hata Mpole ambaye awali hakuwa vizuri, sasa yuko sawa na tayari kwa mechi.
“Wapinzani wetu nao walituambia kuwa watatua nchini jioni ya leo hivyo kila kitu kipo sawa, tunawasubiri kupambana nao kutafuta matokeo na mwisho tusonge mbele kweye michuano hii,” alisema Kivuyo.
Geita ambayo inashiriki kwa mara ya kwanza michuano hiyo ilipoteza mechi hiyo iliyopigwa Uwanja wa Al-Hilal, Khartoum kwa kukubali bao la dakika ya 16 lililofungwa na Omar Ali Naer.
Kimataifa Geita kamili kuikabili Alsahil
Geita kamili kuikabili Alsahil
Green SportsAuthor / Greensports Media LTD
Greensports author
Read also
