London, England
Arsenal imeuanza vyema msimu wa 2022.23 wa Ligi Kuu England (EPL) Ijumaa hii kwa ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Crystal Palace na hivyo kushika usukani wa ligi hiyo ambayo itaendelea Jumamosi na Jumapili kwa timu zote kucheza mechi zao za kwanza.
Ushindi huo wa ugenini unakuwa mwanzo mzuri kwa kocha Mikel Arteta ambaye sasa atakuwa na kazi kubwa na ngumu ya kuhakikisha vijana wake wanaendeleza wimbi hilo la ushindi na hatimaye wanatimiza ndoto ya kulitwaa taji la EPL msimu huu.
Arsenal iliandika bao la kwanza katika dakika ya 20 ya mchezo huo mfungaji akiwa ni Gabriel Martineli ambaye aliitumia vizuri pasi ya Zinchenko bao ambalo liliwapa tabu Crystal Palace kutaka kusawazisha kabla ya kukatishwa tamaa katika dakika ya 85 baada ya Marc Guehi kujifunga na hivyo kuipa Arsenal ushindi wa 2-0.
Ushindi huo mbali na kuwa mwanzo mzuri kwa Arsenal katika EPL lakini pia unaifariji timu hiyo ambayo Aprili mwaka huu ilishindwa kutamba ugenini mbele ya Palace ilipolala kwa mabao 3-0.
Mechi nyingine za mwanzo za ligi hiyo ni kama ifuatavyo…
Jmosi, Agosti 6, 2022
Fulham v Liverpool
Bournemouth v Aston Villa
Leeds United v Wolverhampton
Newcastle v Nottingham Forest
Tottenham v Southampton
Everton v Chelsea
Jpili, Agosti 7, 2022
Leicester v Brentford
Man Utd v Brighton
West Ham v Man City
