Barcelona, Hispania
Klabu ya Barcelona imeingiza faida ya Pauni 86 milioni kwa mwaka wa fedha uliopita na matarajio ni faida hiyo kuongezeka hadi kufikia Pauni 240 milioni kwa mwaka ujao.
Hiyo ni mara ya kwanza kwa klabu hiyo kutengeneza faida tangu kuibuka kwa janga la corona baada ya pato la jumla la klabu hiyo kuongezeka.
Hayo yanakuwa ni mafanikio makubwa kwa klabu hiyo ambayo hapo kabla iliwahi kukwama kusajili wachezaji wapya kwa sababu ya kanuni za matumizi ya fedha za La Liga baada ya kupata hasara iliyofikia Pauni 422 milioni.
Kanuni hizo za matumizi ya fedha ziliifanya klabu hiyo kuchelewa kusajili wachezaji wapya katika majira ya kiangazi kabla ya msimu huu wakiwamo Robert Lewandowski na Raphinha lakini baadaye walichukua hatua kadhaa za kiuchumi kukabiliana na hali hiyo.
Miongoni mwa hatua hizo ni pamoja na kuuza hisa za televisheni na studio ambayo ni sehemu ya kitengo cha habari cha klabu hiyo, hatua ambayo iliwawezesha kujiingizia kipato ambacho kimewasaidia kukidhi matakwa ya matumizi ya fedha kwa mujibu wa kanuni za La Liga na hivyo kuwa huru kufanya usajili wa wachezaji wapya.
Barcelona kwa sasa inashika nafasi ya pili katika La Liga ikiwa na pointi 16 baada ya kucheza mechi sita, ikiwa nyuma ya mahasimu wao, Real Madrid kwa tofauti ya pointi mbili.
Kimataifa Barcelona yaanza kupata faida
Barcelona yaanza kupata faida
Green SportsAuthor / Greensports Media LTD
Greensports author
Read also
