Na mwandishi wetu
Baada ya kuachana na kiungo mshambuliaji Saido Ntibazonkiza, inaelezwa kuwa klabu ya Yanga tayari imekwishafanya maamuzi juu ya nyota wengine watatu wakiongozwa na Deus Kaseke ‘Mwaisa’ ambaye anamaliza mkataba.
Taarifa za ndani kutoka Yanga zinadai kuwa Kocha Mkuu Nasredine Nabi, amepanga kupitisha panga la kutisha mwishoni mwa msimu huu litakaloondoka na rundo la mastaa ambao hawakuwa na mchango mkubwa katika msimu huu.
Na miongoni mwa mastaa walio kwenye ‘red notice’ hiyo ni Deus Kaseke, Abdallah Shaibu ‘Ninja’, Paul Godfrey ‘Boxer’ ambao wanamaliza mikataba huku Yusuph Athuman, David Bryson na fowadi kipenzi cha Wananchi, Heritier Makambo wao wanafikiriwa aidha kuvunja mikataba ama kupelekwa kwa mkopo.
Nabi amesisitiza kuwa anataka kubaki na idadi ndogo ya kikosi walau wachezaji 28 kutoka idadi ya sasa ya wachezaji 31.
Hata hivyo, kutokana na utumishi wake kwa muda mrefu (miaka sita), uongozi wa Yanga umepanga kumuaga kwa heshima Kaseke ambaye tangu atue Jangwani 2015 akitokea Mbeya City amechangia pakubwa ikiwemo kutwaa mataji kadhaa ya Ligi Kuu, Ngao ya Jamii, FA na Mapinduzi.
Soka Kaseke aachwa Yanga
Kaseke aachwa Yanga
Green SportsAuthor / Greensports Media LTD
Greensports author
Read also
