Na mwandishi wetu
Mwamuzi wa kati wa kimataifa wa Tanzania, Jonesia Rukyaa (pichani) na mwamuzi msaidizi, Soud Lila wamevuliwa beji za Fifa na badala yake beji zao wamepewa Amina Kyando wa Morogoro na Mary Seleman wa Dar es Salaam.
Jonesia ambaye alirudishiwa beji mwaka 2023 baada ya kutokuwa nayo kwa miaka miwili kutokana na likizo ya uzazi na Lila kwa pamoja wamefeli mtihani wa utimamu.
Katika orodha iliyowekwa kwenye mtandao wa Fifa, Tanzania ina waamuzi 17 kwa mwaka 2024, kati yao waamuzi wa kati ni sita, wawili ni wanawake na waamuzi wasaidizi tisa, wanawake ni wanne.
Waamuzi wa kati ni Ahmed Arajiga, Ramadhani Kayoko, Hery Sasii na Salum Nasir na Tatu Malogo na Amina Kyando.
Waamuzi wasaidizi ni Frank Komba, Mohamed Mkono, Kassim Mpanga, Ramadhani Ally na Hamdani Said na Janet Balama, Zawadi Yusuf, Glory Tesha na Selemani Mary.
Kwa upande wa waamuzi wa soka la ufukweni ni Jackson Msilombo na Mohamed Ally.
Soka Jonesia, Lila wavuliwa beji za Fifa
Jonesia, Lila wavuliwa beji za Fifa
Green SportsAuthor / Greensports Media LTD
Greensports author
Read also
