Paris, Ufaransa
Nyota wa zamani wa Barcelona, Lionel Messi anaamini kuwa mshambuliaji wa Real Madrid, Karim Benzema ana sifa za kuwa mshindi wa tuzo ya mwanasoka bora wa dunia au Ballon d’Or.
Messi ambaye kwa sasa anaichezea PSG ya Ufaransa na amewahi kutwaa tuzo hiyo mara saba, amesema Benzema amekuwa na msimu mzuri na hivyo hakuna ubishi tuzo hiyo safari hii ni yake.
Benzema akiwa katika msimu wake wa 13 na Real Madrid, msimu huu pekee ameifungia timu hiyo mabao 44 katika mashindano yote na kuisaidia kutwaa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya, Ligi Kuu Hispania au La Liga pamoja na Kombe la Mfalme.
Mshambuliaji huyo pia ndiye kinara wa mabao wa La Liga msimu huu akiwa na mabao 27 lakini pia ndiye kinara wa mabao katika Ligi ya Mabingwa Ulaya huku akikumbukwa kwa kupiga hat trick katika mechi za Real Madrid dhidi ya PSG na Chelsea.
“Hakuna ubishi katika hilo, ni jambo lililo wazi, Benzema amekuwa na mwaka wa kipekee, ameumaliza akiwa mshindi wa Ligi ya Mabingwa na pia amekuwa nguzo katika mechi zote kuanzia hatua ya 16 bora kwenda mbele, nafikiri kwa mwaka huu hakuna shaka kuhusu yeye.” alisema Messi jana akizungumzia mshindi wa Ballon d’Or tuzo itakayotolewa Oktoba 17 na majina ya wanaowania kujulikana Agosti 12.
Akizungumzia mechi yao na Real Madrid ambayo walifungwa mabao 3-2, Messi alisema, “Mechi ya Real Madrid ilituchosha, mimi na karibu kila mtu, inanifanya nitake kushinda tena.”
Hata hivyo Messi alisema timu nzuri si kila mara inashinda kwenye Ligi ya Mabingwa, siwezi kuacha kuwasifia Real Madrid lakini hawakuwa timu nzuri lakini waliweza kumfunga kila mtu.”
Kimataifa Messi: Ballon d’Or ni ya Benzema
Messi: Ballon d’Or ni ya Benzema
Green SportsAuthor / Greensports Media LTD
Greensports author
Read also
