London, England
Baada ya PSG kufanikiwa kumbakisha Kylian Mbappe aliyekuwa akiwaniwa na Real Madrid, vita nyingine ya usajili sasa imehamia England. Liverpool na Chelsea zinapigana vikumbo zikisaka saini ya Ousmane Dembele.
Winga huyo Mfaransa mwenye umri wa miaka 25 anayeichezea Barcelona, alisajiliwa na timu hiyo mwaka 2017 kwa ada ya uhamisho ya Pauni 85 milioni lakini kwa sasa kuna kila dalili kwamba ataondoka katika klabu hiyo.
Kasi ya Liverpool na Chelsea katika kumtaka mchezaji huyo inachangiwa na ukweli kwamba mkataba wake na Barcelona unafikia ukomo baada ya msimu huu majira ya kiangazi na hivyo anatarajia kuwa mchezaji huru.
Liverpool inadaiwa kwamba tayari imeshaanza mazungumzo na wawakilishi wa mchezaji huyo hasa kwa kuwa kocha Jurgen Klopp anadaiwa kuvutiwa na aina ya uchezaji wa Dembele wakati Chelsea nao wanaamini mchezaji huyo atakuwa moja ya usajili mkubwa na wa kwanza wa Todd Boehly, mmiliki mpya mtarajiwa wa klabu hiyo.
Kwa upande mwingine, Liverpool, baada ya kulikosa taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya na lile la England imeamua kuiongezea nguvu safu yake ya ushambuliaji na sasa inamtaka mshambuliaji wa Tottenham, Son Heung-min kutoka Korea Kusini.
Heung mwenye umri wa miaka 29 amekuwa tishio kwa mabao katika msimu uliomalizika wa Ligi Kuu England akifungana na Mohamed Salah wa Liverpool, kila mmoja wao akimaliza msimu akiwa amefunga mabao 23.
Kimataifa Chelsea, Liverpool zamsaka Dembele
Chelsea, Liverpool zamsaka Dembele
Green SportsAuthor / Greensports Media LTD
Greensports author
Read also
