Na mwandishi wetu
Kipa wa KMC, Farouk Shikalo amempongeza kipa wa Yanga, Djigui Diarra kwa kiwango kikubwa anachokionesha kwenye michezo ya Ligi Kuu ya NBC huku akimuhimiza kupambana zaidi ili kufanya kile ambacho wengine walishindwa kukifanya miaka iliyopita.
Shikalo raia wa Kenya aliyeichezea Yanga misimu miwili iliyopita kabla ya kutua KMC mwanzoni mwa msimu huu amesema yeye anapenda kujifunza kwa wazoefu na wanaofanya vizuri, hivyo haoni shida kumsifia mchezaji mwenzake kama anaitendea haki kazi anayoifanya.
“Diarra yuko vizuri, anastahili kuwa bora kwa sababu ya uzoefu mkubwa alionao, ameonesha kusaidia timu yake na pengine anaweza kuifanya timu yake kufikia malengo ambayo wengine tulishindwa.
“Ukiona mtu amekuja, amechukua nafasi yako na kufanya vizuri zaidi yako huna budi kumpongeza, namuombea kwa Mungu apambane ili afanikishe kile kilichokusudiwa,” alifafanua Shikalo aliyewahi kuidakia Bandari ya Kenya.
Shikalo alisema kipa huyo kutoka nchini Mali ana uzoefu na mafanikio makubwa kama ilivyo kwa Juma Kaseja ambaye ni kipa wa KMC pia, hivyo anafarijika kuwaona na kutamani kufika mbali zaidi kwa kufuata nyayo zao za kufanya vizuri na kutimiza malengo yake.
Diarra ni miongoni mwa makipa wanaofanya vizuri msimu huu akiongoza kwa ‘Cleen sheet’ akiwa nazo 15 akiiongoza Yanga kufungwa mabao machache zaidi msimu huu ambayo ni saba.
Soka Shikalo ampongeza Diarra
Shikalo ampongeza Diarra
Green SportsAuthor / Greensports Media LTD
Greensports author
Read also
