Na mwandishi wetu
Namungo jana ilipoteza mchezo wake wa Ligi Kuu ya NBC kwa kulala bao 1-0 mbele ya Dodoma Jiji na sasa benchi la ufundi la timu hiyo linakwenda kujipanga kuhakikisha wanapata matokeo ya ushindi kwenye mechi nne zilizobaki ili kumaliza kwenye nafasi ya tatu.
Kocha msaidizi wa Namungo, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ ameeleza kuwa kufungwa huko ni kutokana na makosa machache lakini wamefurahi kuona kikosi chao kimemiliki sehemu kubwa ya mchezo ingawa walikosa matokeo kwa kuwa ndiyo soka lilivyo.
Julio ameapongeza wapinzani wao kwa ushindani walioutoa kwenye mechi hiyo lakini sasa wamepata nguvu mpya ya kujipanga kupambania nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi katika mechi nne zilizosalia kabla ya kufungwa kwa pazia la Ligi Kuu Bara msimu huu.
“Ukiondoa matokeo, vijana wamejitahidi vya kutosha kumiliki mchezo kwa sababu kipindi cha pili tulimiliki kwa kiasi kikubwa kwa kuwa tulihitaji goli lakini imeshindikana na ndiyo mpira huo lakini bado tuna mechi tunakwenda kujipanga vizuri kuhakikisha azma yetu ya kuingia nne bora inatimia hasa nafasi ya tatu,” alisema Julio.
Hata hivyo, Namungo inashikilia nafasi ya tatu kwa pointi 37 baada ya mechi 26 ikichuana vikali na Azam inayoshikilia nafasi ya nne kwa pointi 35 baada ya mechi 25.
Soka Namungo yajipanga baada ya kipigo
Namungo yajipanga baada ya kipigo
Green SportsAuthor / Greensports Media LTD
Greensports author
Read also
