Na mwandishi wetu
Simba leo imeshindwa kutamba mbele ya Gieta Gold katika Ligi Kuu ya NBC Bara baada ya kutoka sare ya bao 1-1 huku mshambuliaji George Mpole akitamba katika mbio za kusaka ufungaji bora wa ligi hiyo kwa kumpiku Fiston Mayele.
Katika mechi hiyo iliyopigwa kwenye dimba la CCM Kirumba jijini Mwanza, wenyeji Geita ndio waliokuwa wa kwanza kupata bao lililofungwa na Mpole katika dakika ya 20 kabla ya Simba kusawazisha dakika nane baadaye kwa bao lililofungwa na Kibu Dennis.
Matokeo hayo yanazidi kufifisha mbio za Simba katika kukimbizana na mahasimu wao Yanga kuliwania taji la Ligi Kuu Bara msimu wa 2021/22 ambao unafikia ukomo baadaye mwezi ujao.
Baada ya matokeo hayo, Simba inakuwa imecheza mechi 25 sawa na Yanga lakini wakati Yanga wakiwa na pointi 63, Simba wana pointi 51 matokeo ambayo yanaifanya Yanga sasa kubakiwa na mechi mbili ingawa kati ya hizo inaweza kushinda moja na kutoa sare moja kabla ya kutangaza ubingwa.
Kwa maana nyingine Yanga inatakiwa kushinda mechi yake dhidi ya Biashara na baada ya hapo ikitoka sare yoyote na Coastal Union inakuwa bingwa kwani itafikisha pointi 67 ambazo hakuna timu inayoweza kuzifikia ikiwamo Simba.
Wakati Simba ikiwa katika mazingira hayo, mshambuliaji Mpole amezidi kuonyesha makali yake katika mbio za kuhakikisha anabeba tuzo ya mfungaji bora msimu huu kwani hadi sasa anakuwa kinara wa mabao akiwa amefikisha mabao 14 na kumuacha Fiston Mayele wa Yanga mwenye mabao 13.
Kwa kipindi kirefu Mayele amekuwa tishio kwa mabao ikiaminika kwamba msimu huu ni wake kabla ya Mpole kuibuka na kumfikia na sasa inaonekana amekuwa tishio na haitoshangaza akimpiku Mayele na kuwa mfungaji bora msimu huu.
Soka Simba yabanwa, Mpole amtisha Mayele
Simba yabanwa, Mpole amtisha Mayele
Green SportsAuthor / Greensports Media LTD
Greensports author
Read also
