Na mwandishi wetu
Hatimaye leo Kamati ya Utendaji ya Yanga kupitia mwenyekiti wa klabu
hiyo, Dk Mshindo Msolla imemkabidhi kadi ya uanachama msemaji wao,
Haji Manara.
Tukio hilo limefanyika makao makuu ya klabu hiyo mitaa ya Twiga na
Jangwani jijini Dar es Salaam wakati Yanga ikiwa katika maandalizi ya
mchezo wao dhidi ya Simba utakaopigwa Jumamosi hii kwenye Uwanja wa
Mkapa, Dar es Salaam.
Msolla alisema: “Kamati ya utendaji iliridhia Haji kuja kwetu na
ilibariki na niseme tu hongera kwa sababu baada ya Haji kutangaza kuja
upande huu, Wanayanga wote walifurahia, tukajua kumbe maamuzi ya
utendaji yalipata baraka kwa Yanga wote.
“Mengi yalisemwa imekuwaje Haji amekuja lakini imani ya uongozi na
kamati ya utendaji, yeye pia amedhihirisha ni mwenzetu, anafanya kazi
ya weledi na amesaidia kuongeza hamasa kwetu, sasa leo tuna tukio
kubwa la kuwadhihirishia Wanayanga na Watanzania wote kwamba Haji ni
Mwananchi kwa kumkabidhi kadi, hilo ni jambo kubwa kama uongozi kwetu
ni jambo la faraja,” alisema Msolla.
Manara kupewa kadi hiyo ni kama kuzima fununu za kwamba msemaji huyo
alikuwa batili kuwepo Yanga kwa kuwa alitua hapo akitokea Simba kwa
mahasimu wao na kuibua hisia mbalimbali.
Manara aliyefanya kazi Simba kwa miaka sita kama Ofisa Habari
alitangaza kuhamia Yanga Agosti 24, mwaka jana na kuwa miongoni mwa
maofisa wa habari ndani ya kitengo cha habari na mawasiliano cha timu
hiyo.
Tukio lake la kuhamia Yanga liliibua minong’ono kwamba alikuwa na kadi
ya Simba lakini mwenyewe aliibuka na kupinga suala hilo akidai hana
kadi na hivyo hajawahi kuwa mwanachama wa Simba.
Soka Hatimaye Manara apewa kadi Yanga
Hatimaye Manara apewa kadi Yanga
Green SportsAuthor / Greensports Media LTD
Greensports author
Read also
