Istanbul, Uturuki
Kipa wa timu ya soka ya Malatyaspor ya Uturuki, Ahmet Eyup Turkaslan (pichani) amefariki dunia kutokana na tetemeko la ardhi lililotokea Jumatatu iliyopita katika nchi za Syria na Uturuki na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 5000.
“Kipa wetu, Ahmet Eyup Turkaslan amepoteza maisha baada ya kuwa kwenye mjengo ulioanguka, Pumzika kwa amani, hatutokusahau, ulikuwa mtu mzuri,,” ilisema taarifa ya klabu hiyo kupitia mtandao wa Twitter.
Turkaslan mwenye umri wa miaka 28 ameichezea klabu ya Yeni Malatyaspor inayoshiriki ligi daraja la pili mara sita tangu ajiunge nayo mwaka 2021.
Winga wa zamani wa klabu za Everton na Crystal Palace, Yannick Bolasie ambaye kwa sasa anaichezea klabu nyingine ya daraja la pili ya Uturuki ya Caykur Rizespor, alisema, “Pumzika kwa amani kaka Eyup Ahmet Turkaslan.”
Bolasie pia alituma salama za pole kwa familia ya kipa huyo, wachezaji wenzake wa klabu ya Yeni Malatyaspor na kuelezea namna alivyosikitishwa na tukio zima lililomkuta mchezaji huyo hadi umauti.
Winga wa kimataifa wa Ghana anayechezea klabu ya Hatayaspor pia ya Uturuki, Christian Atsu ni kati ya walionusurika katika janga hilo baada ya kupotea kwa siku nzima, baadaye alipatikana akiwa hai.
Kimataifa Tetemeko laua kipa Uturuki
Tetemeko laua kipa Uturuki
Green SportsAuthor / Greensports Media LTD
Greensports author
Read also
