Na mwandishi wetu
Timu ya Dodoma Jiji imejinadi kuwa imefanya marekebisho ya uhakika ndani ya kikosi hicho kuhakikisha inaifumua Azam kwenye mechi yao ya keshokutwa ya Ligi Kuu NBC.
Timu hizo zinakutana ikiwa ni wiki moja imepita tangu walipovaana kwenye mchezo wa hatua ya 32 bora ya Kombe la FA uliopigwa Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam na Azam kupata ushindi wa mabao 4-1.
Kocha msaidizi wa Dodoma, Kassim Liogope amesema kwamba kuelekea mchezo huo utakaopigwa Uwanja wa Jamhuri, Dodoma wamejipanga sawasawa na kurekebisha makosa yaliyowagharimu awali ikiwemo kutotumia kwa ufasaha nafasi za mabao wanazotengeneza.
“Ni mechi mbili tofauti, ya FA ina malengo yake na ligi ina malengo yake kwa hiyo sasa tunatazamia kwenye ligi, mchezo uliopita ulitusaidia kuona namna gani tunaikabili Azam kwenye mechi hii na hii itatusaidia ingawa mechi itakuwa ngumu.
“Kwanza tumerekebisha makosa yaliyotugharimu mara ya mwisho, kwenye mechi kubwa kama hii tunapaswa kuamua matokeo mapema, kinachotusumbua ni namna ya kutumia nafasi na sasa tumeboresha eneo hilo tumekaa sawasawa tuko tayari kupata matokeo,” alisema Liogope.
Katika mechi hiyo, Dodoma itakuwa inapigania kutafuta ushindi wa kwanza kwa Azam msimu huu kwani tayari wameshakutana mara mbili, ukiachana na mechi ya FA, mechi ya kwanza ya ligi, Dodoma ilifungwa mabao 2-1.
Soka Dom Jiji yaipania Azam
Dom Jiji yaipania Azam
Green SportsAuthor / Greensports Media LTD
Greensports author
Read also
