Na mwandishi wetu
Mshambuliaji mpya wa Coastal Union, Guelord Mwamba raia wa Jamhuri ya Demokrasia ya Congo amesema anafurahishwa na uwezo wa kufunga unaoonesha na mshambuliaji wa Yanga, Fiston Mayele na kuzidi kumpa matumaini ya kufanya vizuri akiwa Coastal.
Mwamba aliyetua Coastal hivi karibuni amesema mbali na Mayele, uwepo wa wachezaji wengine kutoka Congo umemfurahisha na anamwombea mema Mayele azidi kufanya vizuri kwa ajili ya kuwaongezea wengine motisha.
“Nafurahi kuwepo Coastal maana naamini ndani ya Ligi Kuu unaweza kuonekana zaidi tofauti na ligi nyingine za nchi za karibu, nafurahi pia hapa kuona uwepo wa Mayele ambaye anafunga sana na sisi tunasikia raha kuona mwenzetu anafanya vizuri.
“Ingawa na mimi ni mshambuliaji lakini nafurahi kuona Mayele akifanya vizuri kama ilivyo kwa Wacongo wengine waliopo hapa Tanzania na wanafanya vizuri pia. Hii inatutia moyo hata sisi wengine ambao wakati wetu ukifika pia tutajitahidi kufanya vizuri zaidi,” alisema Mwamba.
Mwamba aliyetua Coastal akitokea Kakamega Homeboys ya Kenya ameeleza zaidi kuwa licha ya kutua wakati ligi ikiwa kwenye mechi za lala salama, anaamini atatikisa nyavu na kujitangaza zaidi kuelekea msimu ujao.
Mayele (pchani juu) aliyemaliza nafasi ya pili msimu uliopita kwenye orodha ya wafungaji bora nyuma ya George Mpole aliyekuwa akikipiga Geita Gold, kwa sasa ndiye anayeongoza orodha hiyo akiwa na mabao 15.
Soka Straika Coastal amzimia Mayele
Straika Coastal amzimia Mayele
Green SportsAuthor / Greensports Media LTD
Greensports author
Read also
