Paris, Ufaransa
Klabu ya Paris Saint Germain (PSG) ya Ufaransa ilikuwa ikijiandaa kumruhusu mshambuliaji wake, Kylian Mbappe ajiunge na Liverpool wakati wa majira ya kiangazi lakini mchezaji huyo alikataa.
Kwa mujibu wa chanzo kimoja cha habari cha nchini Ufaransa, Mbappe alikataa ofa ya kujiunga na Liverpool wakati huo ili aweze kujiunga na klabu ya Real Madrid ya Hispania ambayo pia ilikuwa ikimtaka.
Mpango wa Mbappe kujiunga na Real Madrid ulikuwa gumzo duniani kote tofauti na ule wa Liverpool ambao inaonekana uliendeshwa kimya kimya na mchezaji huyo hakukubaliana nao na hivyo ukafa kimya kimya .
Kama ambavyo mpango wa kujiunga na Liverpool ulikwama, hata ule wa kwenda Real Madrid nao pia ulikwama na hatimaye mchezaji huyo akaendelea kubaki na vigogo hao wa jiji la Paris hadi sasa.
Habari za ndani zilidai kwamba Rais wa Ufaransa Manuel Macron naye alipenda kuona mshambuliaji huyo ambaye pia anaichezea timu ya Taifa ya Ufaransa akiendelea kucheza soka nchini humo.
Baada ya kumkosa Mbappe, Real Madrid ilimsajili mchezaji mwingine Mfaransa Tchouameni anayecheza nafasi ya kiungo.
Kimataifa Kumbe Mbappe aliikataa Liverpool
Kumbe Mbappe aliikataa Liverpool
Green SportsAuthor / Greensports Media LTD
Greensports author
Read also
