Na mwandishi wetu
Klabu ya Singida Big Stars imeelezwa kumuondoa katika kikosi chake, mchezaji Enock Atta kutokana na suala lake la kibali cha Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) kukwama mpaka sasa.
Atta aliyewahi kuituimikia Azam FC hapo awali, ni miongoni mwa wachezaji waliosajiliwa na Singida BS kwenye dirisha dogo la usajili lililofungwa hivi karibuni akitokea Horoya AC ya kwao Ghana.
Kiungo huyo mshambuliaji alishafika nchini mapema kujiunga na timu hiyo, akitumika pia kwenye baadhi ya michezo ya michuano ya Kombe la Mapinduzi iliyomalizika hivi karibuni visiwani Zanzibar.
Taarifa zinaeleza kuwa Horoya ndiyo imekwamisha mpango wa kukamilisha hati hiyo na kupelekea Singida kumuengua kwenye kikosi chake katika mechi zilizosalia huku juhudi nyingine za kulitatua suala hilo zikiendelea.
GreenSports ilipowatafuta viongozi wa Singida akiwemo Ofisa Habari wao, Hussein Masanza simu yake ya mkononi iliita bila majibu lakini alipotafutwa Ofisa Habari wa TFF, Clifford Ndimbo alitolea ufafanuzi kuhusiana na hilo.
“Usajili wa Atta kidogo una shida maana wao Horoya wamegoma kuitoa ITC yake wakisema bado mchezaji ana mkataba nao hivyo hapo tena hakuna kingine kinachoweza kufanyika labda mpaka dirisha lijalo la usajili na ionekane amemaliza mkataba au wamalizane kwa namna nyingine,” alisema Ndimbo.
Soka Singida Big yamuacha Atta
Singida Big yamuacha Atta
Green SportsAuthor / Greensports Media LTD
Greensports author
Read also
