Na mwandishi wetu
Mshambuliaji wa Yanga, Yacouba Sogne leo Jumamosi amewaaga rasmi viongozi, wachezaji na mashabiki wa timu hiyo kwa namna alivyoishi nao vizuri wakati akiitumikia klabu hiyo.
Yacouba raia wa Burkina Faso ameaga jana kupitia ukurasa wake wa mtandao wake wa kijamii wa Instagram ikifafanulia ni baada ya mazungumzo ya kuongezewa mkataba na timu hiyo kugonga mwamba.
Imeelezwa kuwa Yanga ilikuwa ikifikiria kumjumuisha kikosini nyota huyo ambaye alikuwa na majeraha ya muda mrefu tangu Novemba, 2021 kabla ya kuripotiwa kurejea mazoezini Februari mwaka jana lakini ujio wa Mzambia, Kennedy Musonda umetajwa kuharibu dili lake hilo.
“Ulikuwa wakati mzuri tangu tulipokuwa pamoja mpaka sasa, asanteni kwa upendo wenu kwangu na ushirikiano wenu kuanzia kwa wachezaji hadi uongozi wote wa Yanga na mashabiki. Daima nitawakumbuka hadi wakati mwingine, wananchi ahsante sana na kwaherini, nawapenda,” aliandika Yacouba.
Yacouba alitua Yanga msimu wa 2020-21 akitokea Asante Kotoko ya Ghana na mara ya mwisho kuonekana akiitumikia Yanga ni kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi 2023 iliyomalizika juzi Ijumaa.
Soka Yacouba Sogne aaga Yanga
Yacouba Sogne aaga Yanga
Green SportsAuthor / Greensports Media LTD
Greensports author
Read also
