Na mwandishi wetu
Timu ya Singida Big Stars imejinasibu kuwa inajiandaa vilivyo kuhakikisha kwa mara ya kwanza wanatwaa ubingwa wa Kombe la Mapinduzi kwa kuifunga Mlandege FC, keshokutwa.
Timu hizo zinakutana kwenye fainali hiyo inayosubiriwa kwa hamu kwenye mechi itakayopigwa kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
Kocha msaidizi wa Singida, Mathias Lule alisema jana kuwa licha ya kutinga fainali baada ya kuichapa Azam mabao 4-1 kwenye nusu fainali hiyo haimaanishi kuwa mchezo ujao utakuwa mwepesi bali wanapaswa kujipanga vilivyo kuhakikisha wanachukua ubingwa.
“Tunajiandaa kwa hadhi ya fainali, ni mechi ya mwisho kwa hiyo tunajiandaa kuona namna tunavyoweza kupata matokeo mazuri katika hiyo mechi maana kila mchezo una ugumu wake na ulaini wake.
“Yaani kwa kuwa tumeifunga Azam nne basi na Mlandege pia itakuwa hivyo, hapana, kila mechi tunajiandaa upya na tutaingia kutafuta mabao na kuona namna gani tunaweza kupata matokeo na uzuri tumekuwa na ushirikiano kama timu tukiamini hiyo pia inaweza kutupa ushindi,” alisema Lule.
Singida ambayo inashiriki michuano hii kwa mara ya kwanza, imefika hatua hiyo baada ya kuifunga KMKM mabao 2-0 kisha kutoa sare na Yanga ya bao 1-1 na hivyo kupenya hatua ya nusu fainali kwa uwiano mzuri wa mabao ya kufunga.
Soka Singida Big yataka taji la Mapinduzi
Singida Big yataka taji la Mapinduzi
Green SportsAuthor / Greensports Media LTD
Greensports author
Read also
