Barcelona, Hispania
Kocha wa Barca, Xavi Hernandez amesema mwamuzi wa mechi yao na Espanyol iliyoisha kwa sare ya bao 1-1 alishindwa kuusimamia mchezo.
Katika mechi hiyo au Catalan Derby iliyopigwa Nou Camp jana Jumamosi, utata ulijitokeza baada ya mwamuzi huyo, Antonio Lahoz kuwapa penalti Espanyol katika dakika ya 73 na Espanyol kuitumia vizuri penalti hiyo kupata bao la kusawazisha.
Dakika 10 baada ya penalti hiyo Lahoz alijikuta katika utata zaidi baada ya kutoa kadi saba za njano na nyekundu mbili walizopewa Jordi Alba na Vinicius Souza na kuzifanya timu zote zibaki na wachezaji 10 uwanjani kabla ya kutoa kadi ya tatu nyekundu aliyompa Leandro Cabrera, kadi ambayo baadaye alilazimika kuifuta.
“Leo (jana) ni yeye ndiye aliyeharibu mechi, alikuwa akitoa kadi bila sababu zozote na pia alishindwa kuusimamia mchezo, lakini hilo si kosa lake ni kosa letu tumetoka sare, tumepoteza pointi,” alisema Xavi katika mkutano na waandishi wa habari.
Alipobanwa aeleze nini hasa alichomwambia mwamuzi huyo baada ya filimbi ya kumaliza mchezo kupulizwa, Xavi ambaye pia alipewa kadi alisema, “nilimwambia ameshindwa kusimamia mchezo, akaniambia, unadhani nimeshindwa?”
Hiyo ilikuwa mechi ya kwanza kwa Lahoz tangu kumalizika kwa fainali za Kombe la Dunia za Qatar ambapo mwamuzi huyo pia alilaumiwa kwa namna alivyochezesha mechi ya robo fainali kati ya Uholanzi na Argentina ambao baadaye waliibuka mabingwa wa dunia. Katika mechi hiyo, Lahoz pia alishutumiwa kwa namna alivyokuwa akitoa kadi.
Kimataifa Xavi amshutumu mwamuzi
Xavi amshutumu mwamuzi
Green SportsAuthor / Greensports Media LTD
Greensports author
Read also
