Na mwandishi wetu
Baada ya juzi klabu ya Azam kueleza kuachana na kiungo mshambuliaji, Ibrahim Ajibu huku kiungo huyo akihusishwa na mipango ya kujiunga na Singida Big Stars, uongozi wa timu hiyo umeibuka na kutoa ufafanuzi.
Mwenyekiti wa Singida Big Stars, Ibrahim Mirambo ameeleza leo kuwa hizo zinaweza kuwa tetesi kwa sasa lakini kilichopo tayari wameshapokea ripoti ya kocha wao, Hans Pluijm juu ya usajili na wameanza kuifanyia kazi.
Mbali na hilo, Mirambo pia alieleza hata taarifa za kuachana na mshambuliaji wao, Amissi Tambwe hawezi kuzizungumzia kwa sasa mpaka watakapomaliza mchakato wao na kuweka wazi kila kitu.
“Naweza kusema kwa sasa ni mapema sana kuyazungumzia haya lakini ukweli ni kwamba tumeshapokea ripoti ya kocha kama ilivyo utaratibu na sasa tunaifanyia kazi, ikifika mwisho kila kitu tutaweka wazi kujua nani ametoka na nani ameingia japokuwa haitakuwa usajili wa wachezaji wengi,” alisema Mirambo.
Duru mbalimbali hata hivyo zinaripoti kuwa Ajibu aliyedumu Azam kwa msimu mmoja pekee tayari ameshaingia mkataba wa miaka miwili na walima alizeti hao kwa ajili ya kuongeza ubunifu kutoka eneo la katikati ya uwanja mpaka kwa washambuliaji.
Soka Singida Big yamzungumzia Ajibu
Singida Big yamzungumzia Ajibu
Green SportsAuthor / Greensports Media LTD
Greensports author
Read also
