Na mwandishi wetu
Kocha Mkuu wa KMC, Thierry Hitimana ameeleza kufarijika na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Coastal Union kitu walichokuwa wakikisubiri kwa muda mrefu kwenye Ligi Kuu ya NBC na sasa ni kama wamepata ufunguo kwenye ligi hiyo.
KMC imeibuka na ushindi huo jana kwenye mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam baada ya kushindwa kupata ushindi kwenye mechi zake saba za ligi zilizopita.
“Tunashukuru Mungu kwa ushindi huu, imekuwa kama faraja maana tulipitia kipindi kigumu mno hapa kati, tulikuwa tunahitaji ushindi wowote ili tupate ufunguo wa kuendeleza ushindi, sasa tumepata ingawa ni baada ya kushinda mechi ya Kombe la FA iliyopita (KMC ilishinda 6-1 dhidi ya Tunduru).
“Nafikiri sasa tunahitaji kuendelea kupambana, tunachohitaji kikubwa sasa ni pointi tatu tu na wala sio mabao mengi, tutarejea mazoezini kuendelea kujiweka sawa kwa ajili ya kupata matokeo katika mechi zinazokuja,” alisema Hitimana.
Naye kocha wa Coastal, Yusuf Chippo alisema: “Mchezo umeisha tumepoteza lakini tumecheza vizuri tumetengeneza nafasi ambazo hatukuzitumia na mwishowe tumeadhibiwa, tumesua sua kidogo kwenye ulinzi wakapata bao, tutarejea mazoezini kujiweka sawa, bado tunahitaji kuimarika zaidi.”
Kwa ushindi huo, KMC sasa imepanda kwa nafasi mbili mpaka nafasi ya tisa ikiwa na pointi 19 baada ya mechi 16, Coastal ikisalia nafasi ya 12 ikiwa na pointi 15.
Soka KMC yapata ‘ufunguo’ Ligi Kuu
KMC yapata ‘ufunguo’ Ligi Kuu
Green SportsAuthor / Greensports Media LTD
Greensports author
Read also
