Na mwandishi wetu
Mshambuliaji George Mpole amesema miongoni mwa sababu zilizomuondoa Geita Gold ni kuamini kuwa huu ni muda sahihi wa yeye kutafuta changamoto mpya timu nyingine.
Mpole na Geita walivunja mkataba baina yao jana huku uongozi wa timu hiyo ukimshukuru na kumtakia kila la heri aendako. Hatua hiyo imeibuka baada ya mvutano wa pande hizo mbili kwa zaidi ya wiki sita sasa.
Awali, kulielezwa uwepo wa madai ya Mpole kwa timu hiyo kiasi cha kuondoka kambini kabla ya kuripotiwa kurejea kuendelea na majukumu yake wiki mbili zilizopita kabla ya juzi kutoka tamko la Mpole na Geita kukubaliana kuachana.
“Nimemalizana nao (Geita) sasa naenda kutafuta changamoto sehemu nyingine, ikifika muda sahihi kila kitu kitafahamika kwamba nimeenda wapi ingawa nimeshajua ninapoelekea lakini ikishakuwa imekamilika itakuwa wazi,” alisema.
“Niseme hatukuwa na shida yoyote na Geita kwa sababu pale ni nyumbani, ni familia nishakaa na kufanya kazi kwa vipindi tofauti ila nadhani wakati umefika wa kwenda kutafuta changamoto kwingine kwa sasa sina ninachodaiwa na Geita na wala mimi sina ninachodai,” alisema Mpole.
Nyota ya Mpole iling’aa mno msimu uliopita alipoibuka mfungaji bora akipachika mabao 17 dhidi ya Fiston Mayele wa Yanga aliyefunga mabao 16 na baada ya hapo zilianza kuibuka habari akihusishwa kuwaniwa na klabu kubwa na wakati huo pia uhusiano wake na Geita ulianza kuyumba.
Msimu huu Mpole ameichezea Geita mechi tano na kufunga mabao matatu, ikimuweka mbali kukipigania kiatu chake dhidi ya wanaoongoza kwa mabao mpaka sasa, Mayele na Moses Phiri wa Simba waliofunga mabao 10 kila mmoja.
Soka Mpole asaka changamoto mpya
Mpole asaka changamoto mpya
Green SportsAuthor / Greensports Media LTD
Greensports author
Read also
