Na mwandishi wetu
Kichapo cha mabao 2-1 walichokipata Simba Queens jana kwa JKT Queens kimemchefua kocha mkuu wa timu hiyo, Charles Lukula ambaye ameitupia lawama safu yake ya ushambuliaji kwa kukosa umakini na kushindwa kutumia nafasi walizotengeneza.
Kichapo hicho kimekuwa cha kwanza kwa timu hiyo kwenye uwanja wake wa nyumbani tangu ilipoanza kucheza Ligi Kuu ya Wanawake.
Lukula raia wa Uganda, alisema kulingana na kile kilichoonyeshwa na wachezaji wake hakutegemea kwani hawakucheza kama alivyotarajia kwamba wangejituma zaidi na kuonesha umakini.
“Nina kazi ya kufanya hasa kwenye safu ya ushambuliaji, haikuwa makini, tumetengeneza nafasi nyingi na tumepata penalti tumeshindwa kutumia na hatuna cha kufanya kama tumekosa.
“Nimesikitishwa sana na mtazamo wa wachezaji kwa sababu tungepata angalau pointi moja, sijafurahishwa na uvivu nitaenda kubadili mitazamo yao, wasipokubali nitabaki na wachezaji wachache,” alisema Lukula.
Alisema hakutegemea kuona timu yake ikicheza kwa kukosa umakini na kujiamini kwani wametoka katika mashindano makubwa na kuona hakuna wa kuweza kuwasumbua kwenye mashindano.
Naye Kocha Mkuu wa JKT Queens, Grayson Haule, alisema anawapongeza wachezaji wake kufuata maelekezo aliyowapa ingawa ilikuwa mechi ngumu lakini aliingia uwanjani na kuwaheshimu Simba baada ya kuwafuatilia katika michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika kwa Wanawake ambayo walitoka kuwakilisha ukanda wa Cecafa.
“Nimeona ubora na madhaifu yao na kuyafanyia kazi kwenye mazoezi na wachezaji kufuata ambacho niliwapa na sasa tumepata pointi tatu nyumbani kwa wapinzani wetu. Eneo la kati ndiyo tulifanikiwa kutawala, wana timu nzuri, umakini waliouonyesha Morocco, katika hii ligi yetu hakuna timu ambayo ingeweza kuwashika,” alisema Haule.
Soka Kocha Simba Queens alaumu mastraika
Kocha Simba Queens alaumu mastraika
Green SportsAuthor / Greensports Media LTD
Greensports author
Read also
