Na mwandishi wetu
Kocha wa Azam FC, Kali Ongala ameeleza kufurahishwa na uwezo unaooneshwa na vijana wake baada ya jana Jumatatu kufanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Polisi Tanzania kwenye Uwanja wa Ushirika, Moshi.
Ushindi huo ni wa nane mfululizo kwa Azam kwenye Ligi Kuu Bara, wakikwea nafasi ya pili kwa pointi 35 sawa na vinara Yanga ambao wako juu kwa uwiano mzuri wa mabao ya kufunga na kufungwa.
Ongala alisema anajivunia wachezaji wake kwa ubora wanaoendelea kuuonesha huku kikosi hicho kipana alichonacho kinamfanya asifikirie kusajili kwenye dirisha dogo la usajili kuelekea ngwe ya lala salama.
“Ninajivunia mno kwa vijana wetu, wameonesha ubora maana viwanja vya ugenini huwa ni vigumu kutokana na mazingira, hali ya hewa lakini wamepambana mno sababu hata Polisi wana timu nzuri pia, makosa yetu madogo madogo tunaendelea kuyaweka sawa.
“Kuelekea mzunguko unaofuata watu watarajie ushindani wetu mkubwa na kuhusu kusajili sidhani labda kutokee chochote lakini tuna kikosi kikubwa na wapo wengine wazuri hawajapata nafasi kwa hiyo sidhani kama kutakuwa na lolote, itafahamika,” alisema Ongalla.
Kwa upande wa kocha msaidizi wa Polisi, John Tamba alikiri wachezaji wake kukosa umakini kwenye dakika za kipindi cha kwanza na kupelekea kufungwa bao lakini baadaye walionesha utulivu na kucheza vizuri isipokuwa matokeo hayakufanikiwa kurejea upande wao.
Soka Kocha Azam ajivunia uwezo wa timu
Kocha Azam ajivunia uwezo wa timu
Green SportsAuthor / Greensports Media LTD
Greensports author
Read also
