Na mwandishi wetu
Azam inajifua vikali kuhakikisha inakaa vizuri na kulipa kisasi kwa Coastal Union katika mechi yake ya Ligi Kuu NBC itakayopigwa Jumapili hii.
Azam inayonolewa na Kally Ongala, mbali na kuutaka ushindi kwa Coastal, pia inataka kujifuta machozi baada ya kutolewa kwenye nusu fainali ya Kombe la FA na timu hiyo msimu uliopita lakini pia kutimiza ahadi yao ya kushinda mechi zote zilizobaki za mzunguko wa kwanza.
Akizungumza na GreenSports, Kaimu Ofisa Habari wa Azam, Hashim Ibwe amesema wanafahamu ugumu wa Caostal na namna gani wamekuwa na matokeo mazuri dhidi yao kila wanapokutana lakini sasa watahakikisha wanalimaliza hilo kwenye mchezo huo utakaopigwa Uwanja wa Azam, Dar es Salaam.
“Tumeanza mazoezi tangu jana tuliposhinda kwa Namungo lakini hilo limepita na sasa tunajipanga dhidi ya Coastal, tunajua ni mechi ngumu, wana kikosi kizuri na walitutoa Kombe la FA msimu uliopita kwa hiyo sasa ni sehemu yetu ya kulipa kisasi.
“Lakini pia lengo letu ni kushinda mechi zote mpaka tunamaliza mzunguko wa kwanza ili tukianza ya pili tuanze kwa ubora ule tuliomaliza nao maana nasi ni miongoni mwa timu zinazoongoza ligi, tofauti ni uwiano wa mabao ya kufunga na kufungwa tu,” alisema Ibwe.
Wakati Azam ikiingia kwenye mechi hiyo ikiwa na ushindi wa mechi tano mfululizo wakati Coastal imefungwa mechi mbili mfululizo lakini kwenye mechi tano za mwisho timu hizo kukutana Azam imeshinda mara moja, Coastal imeshinda mbili na wametoka sare mbili.
Soka Azam yapania kulipa kisasi Coastal
Azam yapania kulipa kisasi Coastal
Green SportsAuthor / Greensports Media LTD
Greensports author
Read also
