Doha, Qatar
Klabu ya Barcelona ndiyo inayoongoza kuwa na wachezaji wengi Qatar kwenye fainali za Kombe la Dunia ikiwa na wachezaji 17 ikifuatiwa na Bayern Munich yenye wachezaji 16 ambayo pia ingeweza kuwa na wachezaji 17 kama Sadio Mane asingeumia.
Barca nayo pia ingekuwa na wachezaji 16 na kuwa sawa na Bayern lakini hali ilibadilika baada ya Alejandro Balde kuitwa katika timu hiyo akichukua nafasi ya Jose Gaya wa Valencia na hivyo kuifanya timu hiyo kuwa na wachezaji 17 walioko kwenye fainali hizo zilizoanza jana Jumapili na kufikia tamati Desemba 18.
Mane, mshambuliaji wa timu ya Senegal anayeichezea klabu ya Bayern Munich, aliondolewa katika kikosi cha Senegal katika hatua za mwisho baada ya vipimo kuonyesha kwamba asingeweza kupona na kucheza japo mechi moja ya timu hiyo.
Awali ilielezwa kwamba mchezaji huyo bora wa Afrika angekosa mechi moja na baada ya hapo angekuwa vizuri kuiwakilisha Senegal katika mechi nyingine mbili za hatua ya makundi ambazo zingeaua hatma ya timu hiyo kama ni kufuzu hatua ya mtoano au kuaga michuano.
Orodha ya wachezaji wa Barca na timu za Taifa wanazochezea wachezaji hao zikiwa kwenye mabano ni kama ifuatavyo…
Raphinha (Brazil), Marc-Andre ter Stegen (Ujerumani), Frenkie de Jong (Uholanzi), Memphis Depay (Uholanzi), Ferran Torres, Sergio Busquets, Jordi Alba, Alejandro Balde, Eric Garcia, Gavi, Pedri, Ansu Fati (Hispania), Andreas Christensen (Denmark), Ronald Araujo (Uruguay), Robert Lewandowski (Poland) na Ousmane Dembele na Jules Kounde wa Ufaransa.
Wachezaji wa Bayern waliopo Qatar ni Choupo-Moting (Cameroon), Noussair Mazraoui (Morocco)Serge Gnabry, Thomas Muller, Jamal Musiala, Manuel Neuer, Leroy Sane, Leon Goretzka, Joshua Kimmich (Ujerumani), Alphonso Davies (Canada), Matthijs de Ligt (Uholanzi) na Josip Stanisic (Croatia) na Dayot Upamecano, Benjamin Pavard, Kingsley Coman, Lucas Hernandez wa timu ya Ufaransa.
Kimataifa Barca watawala Kombe la Dunia
Barca watawala Kombe la Dunia
Green SportsAuthor / Greensports Media LTD
Greensports author
Read also
