Na mwandishi wetu
Timu ya soka ya Yanga inatarajiwa kusafiri kesho Jumapili alfajiri kuelekea Singida kwa ajili ya mchezo wao dhidi ya Dodoma Jiji utakaochezwa Jumanne.
Akizungumzia safari hiyo, meneja wa kikosi hicho, Walter Harrison alisema kulingana na mazoezi ya siku mbili hakuna mchezaji majeruhi, hata Fiston Mayele aliyeumia katika mchezo uliopita dhidi ya Singida Big Stars amejiunga na wenzake kwa maandalizi ya mchezo huo.
Alisema Mayele alishiriki kwenye mazoezi ya gym jana akiwa na wachezaji wenzake na kuonesha hali yake kwa sasa imeimarika na yuko tayari kuungana na wenzake katika safari ya Singida.
“Timu imefanya mazoezi ya gym na kucheza mechi ya mazoezi na timu ya vijana kwenye Uwanja wa Avic Town, baada ya hapo timu itasafiri na ndege kuelekea Dodoma na baada ya hapo tutaunga na basi kuelekea Singida,” alisema Harrison.
Yanga ambayo iliibuka na ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Singida Big Stars, wataingia kwenye mechi hiyo itakayopigwa kwenye Uwanja wa Liti wakiwa na morali ya juu baada ya kuonesha kiwango bora katika mchezo na Singida uliopigwa Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam.
Katika mech ya msimu uliopita Yanga ilichukua pointi sita kutoka kwa Dodoma Jiji, ikishinda ugenini mabao 2-0 na nyumbani ikaibamiza mabao 4-0.
Soka Yanga yaifuata Dodoma Jiji
Yanga yaifuata Dodoma Jiji
Green SportsAuthor / Greensports Media LTD
Greensports author
Read also
