Na mwandishi wetu
Sakata la mshambuliaji wa Geita Gold, George Mpole limechukua sura mpya baada ya kuelezwa kuwa mchezaji huyo amekubali kukutana na uongozi wa timu hiyo kumaliza tofauti zilizopo kati yao.
Hayo yameelezwa Alhamisi hii na Katibu Mkuu wa Geita, Ramadhani Bukambu ambaye alifafanua kwamba wamewasiliana na mfungaji huyo bora wa msimu uliopita aliyepachika mabao 17 na amekubali kwenda Geita kuzungumza kwa kina yanayomsibu.
“Tumezungumza naye na hata leo asubuhi nimetoka kuwasiliana naye, tumeelewana kwamba atakuja huku pamoja na timu maana yeye yupo Mbeya na timu imeenda Mbeya kwa hiyo wakimaliza mechi (dhidi ya Mbeya City) naye atakuja na kikosi.
“Nimemweleza na amenielewa kwamba kama kuna kitu hakiendi sawa basi atakuja hapa tukifahamu, tuzungumze na tujue imekuwaje mwisho tupate suluhu katika hili, kwa hiyo baada ya hapo nafikiri kutakuwa na mwafaka,” alisema Bukambu.
Mpole alitajwa kutoweka Geita baada ya mechi yao na Coastal Union kwa kile alichoeleza kuwa anaumwa huku taarifa nyingine zikidai kwamba nyota huyo anadai stahiki zake ikiwemo mshahara wake wa mwezi Oktoba.
Taarifa za madai zilikanushwa na uongozi wa Geita, wakifafanua kuwa walishamlipa stahiki zake zote isipokuwa mshahara wa Oktoba ambao walidai hakuufanyia kazi.
Soka Mpole, Geita wakaa mezani
Mpole, Geita wakaa mezani
Green SportsAuthor / Greensports Media LTD
Greensports author
Read also
