Manchester, England
Kiungo wa Man United, Bruno Fernandes amehoji fainali za Kombe la Dunia kufanyika kipindi hiki na kuelezea masikitiko yake kuhusu vifo vya wafanyakazi wahamiaji zaidi ya 6,000 waliohusika katika ujenzi wa viwanja vya soka vya Qatar vitakavyotumika kwenye fainali hizo.
Fainali za Kombe la Dunia zitaanza rasmi Novemba 20 lakini Fernandes ambaye ataiwakilisha Ureno kwenye fainali hizo amehoji kitendo cha michuano hiyo kufanyika mara ya kwanza katika majira ya baridi Ulaya na kuwapo habari za vifo vya watu zaidi ya 6,000 vilivyotokea wakati wa ujenzi wa viwanja saba, ingawa mamlaka za Qatar zimepinga kutokea idadi hiyo ya vifo.
“Ni wazi kwamba si wakati ambao tunataka fainali za Kombe la Dunia zifanyike, nafikiri kila mmoja, wachezaji na mashabiki, si wakati mzuri, watoto watakuwa shule, watu watakuwa kazini na muda hautokuwa mzuri kwa watu kuangalia mechi,” alisema Fernandes.
“Tunajua mazingira yanayozunguka fainali za Kombe la Dunia, nini kimetokea wiki chache zilizopita, miezi michache iliyopita, nikuhusu watu ambao wamekufa kwenye shughuli za ujenzi wa viwanja, hatuna raha kwa mambo yote hayo,” alisema mchezaji huyo.
“Tunataka soka liwe kwa kila mtu, kila mtu ni lazima ajumuike na kuhusika na Kombe la Dunia kwa sababu ni michuano ya dunia lakini kwa Kombe la Dunia ni zaidi ya soka, ni sherehe kwa mashabiki, wachezaji, ni kitu kinachofurahisha kuangalia, kwa hivyo ni lazima michuano ifanyike katika mazingira mazuri,” aliongeza.
Kimataifa Fernandes ahoji Kombe la Dunia Qatar
Fernandes ahoji Kombe la Dunia Qatar
Green SportsAuthor / Greensports Media LTD
Greensports author
Read also
