Mancheter, England
Kocha wa Manchester City, Pep Guardiola ameiambia mahakama kuwa mchezaji wake, Benjamin Mendy anayekabiliwa na tuhuma za kubaka wasichana na udhalilishaji wa kijinsia, alikuwa kijana mzuri ingawa hajui nini alikuwa akikifanya katika muda wake wa mapumziko.
Mendy amekana makosa saba ya kubaka na moja la kusudio la kubaka pamoja na kosa jingine la udhalilishaji kijinsia matukio anayodaiwa kuwafanyia wasichana sita.
Akitoa ushahidi wake katika Mahakama ya Chester Crown jana Jumatatu, Pep alisema kwamba mchezaji huyo alikuwa akipendwa lakini yeye kama kocha hajui nini alikuwa akikifanya katika muda wake wa mapumziko. “Mimi si baba yake,” aliongeza Pep.
Wakati akihojiwa na wakili wa Mendy, Pep alisema kwamba yeye si mtu anayetumia muda mwingi kwenye mitandao ya kijamii na hana anachojua kuhusu kile akifanyacho Mendy katika muda wake wa mapumziko.
Pep alifafanua kwamba hakuweza kuwasimamia wachezaji wote 22 wa kikosi cha kwanza na badala yake alichokuwa akikiangalia kwa Mendy ni uchezaji wake wa soka.
Awali Mendy aliiambia mahakama kwamba aliwahi kuvunja kanuni zilizowekwa wakati wa kipindi cha janga la korona za kuzuia mikusanyiko kwa kufanya sherehe nyumbani kwake Prestbury, Cheshire zaidi ya mara moja na katika hilo, Pep alisema kwamba mchezaji huyo alikiri kufanya kitu kisicho sahihi.
Baada ya hapo, Pep aliulizwa kuhusu tuhuma za ubakaji zinazomkabili mchezaji huyo ambapo aliiambia mahakama, “Nimeambiwa nije hapa na nyinyi wote na hiyo ndiyo sababu niko hapa.”
Katika mashitaka yanayomkabili, Mendy anadaiwa akiwa na rafiki yake Louis Saha Matturie waliwabaka wasichana kadhaa nyumbani kwa mchezaji huyo jijini Manchester. Mendy na Matturie wote walikana kuhusika na matukio hayo na kusisitiza kwamba kama kuna chochote walichofanyiwa wasichana hao ilikuwa ni kwa makubaliano.
Kimataifa Pep amtetea Mendy mahakamani
Pep amtetea Mendy mahakamani
Green SportsAuthor / Greensports Media LTD
Greensports author
Read also
