London, England
Arsenal imerejea kileleni katika Ligi Kuu England (EPL) baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 katika mechi iliyochezwa leo kwenye dimba la Stamford Bridge.
Ushindi huo uliotokana na bao pekee la Gabriel katika dakika ya 63 unaifanya Arsenal kufikisha pointi 34 wakati Man City yenye pointi 32 na ambayo kabla ya mechi ya Arsenal ishna Chelsea ilikuwa ikishika usukani sasa inashuka hadi nafasi ya pili baada ya kushika usukani kwa muda usiozidi saa 24. Timu zote hizo zimecheza mechi 13 hadi sasa.
Bao hilo pekee lilitokana na mpira wa kona uliopigwa na Bukayo Sako kutokea upande wa kulia baada ya wenyeji Chelsea kushindwa kuuzuia mpira huo.
Macho ya baadhi ya mashabiki yalielekezwa kwa nahodha wa zamani wa Arsenal, Pierre-Emerick Aubameyang ambaye aliihama timu hiyo baada ya kutofautiana na kocha Mikel Arteta na kujiunga na Barcelona Januari mwaka huu lakini mapema mwanzoni mwa msimu huu akajiunga na Chelsea.
Aubameyang ambaye akiwa Arsenal alivuliwa unahodha na Arteta kwa utovu wa nidhamu, alishindwa kuinusuru Chelsea na kichapo na kiujumla mechi haikuwa nzuri kwake kwani aliishia kupewa kadi ya njano kwa kucheza rafu ya waziwazi kabla ya kutolewa katika dakika ya 63 na nafasi yake kuingia Armando Broja.
Ushindi huo ni dalili nyingine nzuri ya Arsenal kutwaa taji la ligi msimu huu au kuhakikisha inakuwa katika top four baada ya kuwa katika nafasi hiyo mara ya mwisho mwaka 2016, matumaini hayo yanatokana na mwenendo mzuri wa timu hiyo ikiwa tayari imeshazibwaga Tottenham na Liverpool ingawa ilishindwa kutamba mbele ya Man United baada ya kulala kwa mabao 3-1.
Kimataifa Arsenal yaipiga Chelsea, yarudi kileleni
Arsenal yaipiga Chelsea, yarudi kileleni
Green SportsAuthor / Greensports Media LTD
Greensports author
Read also
