Na mwandishi wetu
Timu ya Simba SC ambayo imerejea mazoezini juzi kujiwinda dhidi ya Singida Big Stars imefunguka kufahamu ugumu wa mchezo huo unaotokana na ukubwa wa wachezaji wanaoiunda Singida.
Meneja Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally amesema uwa watakwenda mkoani Singida kwa ajili ya mechi hiyo ya Novemba 9 mapema wakitarajia kuanza safari yao mwishoni mwa wiki hii.
Aidha, ofisa huyo alibainisha pia kuelekea mechi hiyo kikosi chao kitakuwa kamili baada ya kurejea kikamilifu kwa wachezaji wao Sadio Kanoute na Augustine Okrah aliyekuwa na hatihati kuelekea mchezo huo.
“Baada ya mechi na Mtibwa Sugar, kikosi kilipumzika kwa siku mbili na Jumatano kikaanza mazoezi na mwishoni mwa wiki tunatarajia kuanza safari ya kuelekea Singida kwa ajili ya mechi dhidi ya Singida.
“Waliosalia majeruhi kuelekea mchezo huo ni Jimmyson Mwanuke na Israel Mwenda lakini wengine waliosalia wako vizuri, mechi ya mwisho tulimkosa Kanoute alikuwa hajapona vizuri na hata Okrah naye yuko poa kikosini kwa hiyo tutaelekea Singida tukiwa timamu asilimia 100.
“Lakini niseme kiujumla mchezo wetu na Singida ni mgumu kwa sababu pamoja na ukweli kwamba ni timu ndogo na mpya lakini ina wachezaji wenye uzoefu ukitazama wanaoiunda Singida ni wachezaji wenye kariba na uzoefu mkubwa, maana yake tunakwenda kucheza mechi ngumu,” alisema Ally.
Soka Simba wakiri, Singida Big wagumu
Simba wakiri, Singida Big wagumu
Green SportsAuthor / Greensports Media LTD
Greensports author
Read also
