Madrid, Hispania
Mechi za makundi Ligi ya Mabingwa Ulaya zimekamilika jana Jumatano usiku, timu 16 zimefuzu hatua ya mtoano, nane zimeangukia Europa Ligi na nane nyingine zikiwamo Atletico Madrid, Rangers na Celtic zikiaga michuano ya Ulaya msimu huu…
Mchuano mkali wa hatua ya makundi ulikuwa Kundi D, Tottenham Hotspur iliyokuwa njia panda iliokolewa kwa bao la dakika za nyongeza na kuifanya itoke na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Marseille na hatimaye kushika usukani wa kundi hilo ikifikisha pointi 11 dhidi ya pointi 10 za Eintracht Frankfurt iliyoshika nafasi ya pili.
Benfica nayo pia ilifanya maajabu Kundi H ikiwa inachuana na Paris Saint Germain (PSG) kuwania kushika usukani wa kundi hilo lakini iliokolewa na ushindi wa mabao 6-1 ulioupata kwa Macabi Haifa na kuongoza kundi hilo ikineemeka kwa faida ya mabao ya ugenini baada ya timu hizo zote kumaliza mechi zikiwa sawa kwa kila kitu ikiwamo pointi, kila moja imefikisha pointi 14.
Kwa timu zilizoaga michuano ya klabu barani Ulaya msimu huu, gumzo kubwa limekuwa kwa kocha Diego Simeone wa Atletico ambaye hatma yake katika timu hiyo imeanza kujadiliwa.
Orodha ya timu mbili zilizofuzu hatua ya mtoano kwa kila kundi na zilizoangukia Europa Ligi ni kama ifuatavyo…
Kundi A
Napoli
Liverpool
Ajax (Europa)
Kundi B
FC Porto
Club Bruges
Bayer Leverkusen (Europa)
Kundi C
Bayern Munich
Inter Milan
Barcelona (Europa)
Kundi D
Tottenham
Eintracht Frankfurt
Sporting Lisbon (Europa)
Kundi E
Chelsea
AC Milan
Salzburg (Europa)
Kundi F
Real Madrid
Leipzig
Shakhtar Donetsk (Europa)
Kundi G
Manchester City
Borussia Dortmund
Sevilla (Europa)
Kundi H
Benifica
Paris Saint Germain
Juventus (Europa)
Timu nane zilizoaga michuano ya klabu Ulaya msimu huu ni kama ifuatavyo…
Atletico Madrid
Rangers
Celtic
Viktoria Plzen
Marseille
Dinamo Zagreb
FC Copenhagen
Macabi Haifa
Matokeo mechi za jana Jumatano Ligi ya Mabingwa Ulaya…
Chelsea 2-1 Dinamo Zagreb
AC Milan 4-0 Red Bull Salzburg
Real Madrid 5-1 Celtic
Shakhtar Donetsk 0-4 RB Leipzig
FC Copenhagen 1-1 B. Dortmund
Man City 3-1 Sevilla
Juventus 1-2 PSG
Maccabi Haifa 1- 6 Benfica
