London, England
Kocha wa Crystal Palace, Patrick Vieira ambaye ni kocha pekee mwenye asili ya Afrika katika Ligi Kuu England (EPL) amesema juhudi zinatakiwa kufanywa ili wachezaji ‘weusi’ wenye asili ya Afrika waingie katika kazi ya ukocha.
Vieira ametoa kauli hiyo wakati kukiwa na ripoti inayodai kwamba asilimia 43 ya wachezaji katika EPL ni wenye asili ya Afrika wakati asilimia 34 ya wachezaji hao hao wapo kwenye Ligi Daraja la Kwanza (EFL) lakini makocha ni asilimia 4.4 tu.
“Ni lazima tuwape fursa watu wa rangi tofauti, tuko vizuri kama mtu mwingine yeyote na tunahitaji kuwa na fursa si nyingi au ndogo kuliko mtu mwingine yeyote, unapoangalia katika ligi tano kubwa duniani na ukiangalia namba ya watu wa Afrika (weusi) katika makocha wengi wanakuwa katika daraja la kwanza na la pili, haitoshi,” alisema Vieira katika mazungumzo yake na BBC.
“Kuna kukosekana kwa fursa, hakuna muunganiko kwa watu wa Afrika wachezaji kujiunganisha sisi wenyewe na kuwa karibu kidogo na watu wenye maamuzi,” aliongeza Vieira.
“Lakini kwa ujumla naamini milango haiko wazi kwa ajili yetu kuingia katika uongozi, nikizungumzia uongozi namaanisha timu, lakini pia nazungumzia katika kiwango cha juu pia, tunahitaji kupewa fursa zaidi kuonyesha kwamba tuko vizuri kama mtu mwingine yeyote,” alisema.
Kabla ya kuwa kocha, Vieira alitamba akiwa mchezaji wa Arsenal na timu ya Taifa ya Ufaransa ambapo alitwaa Kombe la Dunia mwaka 1998 na lile la Ulaya mwaka 2000 wakati katika Arsenal alishinda taji la EPL mara tatu na alikuwa katika timu ambayo msimu wa 2003-04 haikupoteza hata mechi moja kabla ya kutimkia Juventus ambapo alishinda taji la Serie A mara tano.
Kimataifa Vieira ataka makocha Waafrika EPL
Vieira ataka makocha Waafrika EPL
Green SportsAuthor / Greensports Media LTD
Greensports author
Read also
