Na mwandishi wetu
Shirikisho la Soka Afrika (Caf) limetangaza hatua ya mwisho ya mechi za mtoano kwa ajili ya kuingia hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika ambapo Yanga imepangwa kucheza na wababe wa Tunisia, Club Africain.
Droo hiyo iliyochezeshwa muda mfupi uliopita makao makuu ya Caf nchini Misri, imejumuisha timu zilizotoka kwenye hatua ya pili ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika na zile zilizopenya kwenye hatua ya pili ya awali ya Kombe la Shirikisho.
Yanga ambayo leo mchana imetangaza kuingia mkataba wa miezi sita na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (Unicef) unaolenga kuongeza uelewa kwa umma kuhusu janga la Corona na Ebola, itaanzia nyumbani kwenye mchezo huo utakaopigwa Novemba 2 kabla ya mechi ya marudiano Novemba 9, mwaka huu.
Mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu ya NBC walijikuta wakiangukia Kombe la Shirikisho baada ya Jumapili iliyopita kufungwa ugenini bao 1-0 na Al Hilal ya Sudan na hivyo kuondoshwa kwa jumla ya mabao 2-1 baada ya sare ya bao 1-1 kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam.
Club Africain yenyewe iliisambaratisha Kipanga FC ya Zanzibar kwa mabao 7-0 kwenye mechi ya Jumapili iliyopita baada ya suluhu ya kwenye mechi ya awali iliyopigwa kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar.
Soka Yanga kuikabili Club Africain Shirikisho
Yanga kuikabili Club Africain Shirikisho
Green SportsAuthor / Greensports Media LTD
Greensports author
Read also
