Na mwandishi wetu
Bondia wa uzito wa kati, Twaha Kassim ‘Kiduku’ ametamba kuwa ataonesha kiwango na ngumi nzuri kwenye pambano lake la kuwania Mkanda wa WBF dhidi ya Muargentina, Damien Bonelli.
Kiduku amesema kwamba si yeye tu atakayetoa burudani na ushindi mkubwa siku hiyo bali hata Abdallah Pazi ‘Dulla Mbabe’ pia atapambana kuleta heshima dhidi ya mpinzani wake Mbiya Kanku kutoka Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.
Kwa mujibu wa waandaaji wa mapambano hayo, Mo Green International wameeleza kuwa yanatarajia kufanyika Novemba 25, mwaka huu kwenye Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.
“Niwaambie tu mashabiki na wadau kwamba kutakuwa na ngumi kali sana siku hiyo, ambapo mbali na pambano langu ninalojipanga kuendeleza ushindi wangu mfululizo lakini pia kaka yangu Dulla Mbabe naamini atapigana shoo shoo dhidi ya Kanku, siku hiyo naamini itakuwa shoo shoo na burudani kubwa kwa ajili ya watu wa Morogoro na Watanzania wote,” alisema Kiduku.
Bonelli mwenye rekodi ya kucheza mapambano 35, ameshinda mara 24 na kupoteza mara 11 huku akishika nafasi ya 252 kidunia atapigana na Kiduku kwa raundi 10 wakati Kanku anayeshika nafasi ya 254 amepigana mara 17, akishinda 10 na kupoteza sita atapigana na Mbabe kwa raundi nane kwenye pambano lisilo la ubingwa.
Mbali na hilo, bondia maarufu kwa sasa nchini, Karim Mandonga atanyukana na mkongwe Said Mbelwa ‘Moto wa Gesi’ kwenye pambano la raundi sita.
Ngumi Kiduku atamba kumchapa Muargentina
Kiduku atamba kumchapa Muargentina
Green SportsAuthor / Greensports Media LTD
Greensports author
Read also
