London, England
Klabu ya Manchester City imetozwa faini ya Pauni 260,000 na FA kwa kitendo cha mashabiki wake kuingia katikati ya Uwanja wa Etihad kufurahia ushindi wa taji la Ligi Kuu England msimu uliopita.
Mei mwaka huu mashabiki wa Man City waliingia uwanjani kwa kulazimisha mara baada ya timu yao kuifunga Aston Villa mabao 3-2 katika mechi yao ya mwisho ambapo katika tukio hilo, kipa wa Villa, Robin Olsen alibughudhiwa na mashabiki hao ambao pia walivunja mwamba wa goli uwanjani hapo.
Sambamba na adhabu, klabu hiyo pia imeonywa kuwa makini na matukio ya aina hiyo kwa siku zijazo kwa kile ambacho FA imedai kuwa ni kushindwa kuwatuliza mashabiki wao na kuhakikisha wanajiweka kando na vitendo vyovyote vya ghasia na ukosefu wa utulivu uwanjani.
Baada ya tukio hilo, polisi wa Manchester walidai kwamba watu wawili walikamatwa kwa kosa la kuingia katikati ya uwanja na baadaye Julai wakatoa taarifa nyingine wakidai kufanya uchunguzi kuhusu matukio kadhaa ya uhalifu wa kijinai ikiwamo uharibifu wa mali.
Katika mechi hiyo, Man City ilipambana na kupata mabao matatu katika dakika tano baada ya kuwa nyuma kwa mabao 2-0 zikiwa zimebakia dakika 15 mpira kumalizika na kupata ushindi uliowawezesha kubeba taji hilo lililokuwa pia likiwaniwa na Liverpool waliopishana nao kwa tofauti ya pointi moja.
Sambamba na Man City, klabu ya Everton pia imetozwa faini ya Pauni 300,000 kwa matukio mawili ya mashabiki kuingia uwanjani katika mechi ya Ligi Kuu England msimu uliopita dhidi ya Crystal Palace.
Hivi karibuni, klabu za Ligi Kuu England zilitoa taarifa ya kuwaonya mashabiki wenye tabia zisizo za kiungwana au wanaojihusisha na matukio ya kijinai kuwa watapewa adhabu ya kutohudhuria mechi za klabu zao kwa kipindi cha mwaka mmoja.
Kimataifa Mashabiki waiponza Man City, yapigwa faini
Mashabiki waiponza Man City, yapigwa faini
Green SportsAuthor / Greensports Media LTD
Greensports author
Read also
