London, England
Nahodha wa zamani wa Man Utd, Roy Keane ameilaumu klabu hiyo kwa kutompa heshima Cristiano Ronaldo kwa kitendo cha kumsugulisha benchi.
Ronaldo ambaye ameanza mechi moja tu ya Ligi Kuu England msimu huu hakucheza mechi ya Jumapili dhidi ya Man City ambayo Man United ililala kwa mabao 6-3 lakini kocha Erik ten Hag alisema baadaye kwamba uamuzi wa kumuweka Ronaldo benchi ni kwa ajili ya kumlindia heshima.
Keane ambaye amewahi kucheza na Ronaldo Man United hata hivyo alisema kwamba kinachosemwa na Ten Hag hakina ukweli wowote badala yake kinyume chake ndio ukweli na kwamba ni bora klabu hiyo ingemruhusu mchezaji huyo aondoke wakati wa majira ya kiangazi.
Akizungumza jana mara baada ya mechi hiyo, Keane alisema, “Nafikiri Man Utd inachofanya ni kutomheshimu Ronaldo, nafikiri wangemuacha tu aondoke kabla hata ya dirisha la usajili.
“Nafikiri kocha anataka tu kumzuia, ndio ni kweli kwamba anataka kuwa na uteuzi mpana wa wachezaji lakini hawezi kumzuia Ronaldo ili amuweke benchi, ni mmoja wa wachezaji wakubwa kuwahi kutokea, hili wazo kwamba kocha hakuwa na namna ni upuuzi, alikuwa na nafasi hiyo, alikuwa na wachezaji wanne au watano,” alisema.
“Ni kweli kocha alimpa nafasi (Anthony) Martial na akafunga mabao mawili, kwa hiyo mabadiliko hayo yana uhalali lakini ukiangalia kwa mapana hatompa nafasi ya kucheza Ronaldo, tunalijua hilo, amecheza mwanzo katika mechi moja au mbili za Ulaya,” aliongeza Roy Keane.
Kimataifa Roy Keane apinga Ronaldo kusugua benchi
Roy Keane apinga Ronaldo kusugua benchi
Green SportsAuthor / Greensports Media LTD
Greensports author
Read also
