Na mwandishi wetu
Baada ya jana kuambulia sare ya 1-1 dhidi ya Geita Gold, kocha wa Singida Big Stars, Hans van Der Pluijm amebainisha kilichowaangusha kuwa ni safu yake ya ushambuliaji kushindwa kutumia nafasi walizokuwa wakitengeneza.
Singida ilipata sare hiyo ya pili mfululizo kwenye Ligi Kuu ya NBC katika mchezo huo uliopigwa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Pluijm alifafanua kwamba kuhusu kufungwa bao la mapema lilitokana na makosa ya ulinzi ambayo lazima yafanyike ndiyo mpinzani apate bao lakini kuhusu kushindwa kupata ushindi ni suala ambalo atakwenda kulifanyia kazi mara moja ili waendelee na safari yao salama.
“Kufungwa bao mara nyingi huwa ni makosa ya hesabu za ulinzi na pengine kama si hivyo labda tungepata ushindi lakini kwa ujumla nitakwenda pia kuzungumza na wachezaji wangu kuhusu makosa haya maana ndiyo kazi yangu.
“Ila kuhusu kupata mabao, tulitengeneza nafasi kadhaa lakini tulikuwa tunasubiria sana kupeleka mipira sehemu muhimu na wakati mwingine kulifanyika vitu vingi kabla ya kutaka kufunga na hiyo inatengeneza mazingira magumu ya kushinda,” alisema Pluijm.
Kwa matokeo hayo, Singida iliyopanda kushiriki Ligi Kuu msimu huu, imeng’ang’ana kwenye nafasi ya tano kwa pointi zake nane baada ya kushinda michezo miwili ya awali.
Soka Pluijm alia na mastraika Singida Big
Pluijm alia na mastraika Singida Big
Green SportsAuthor / Greensports Media LTD
Greensports author
Read also
