New York, Marekani
Bondia, Floyd Mayweather amesema kwamba anataka kupigana na Conor McGregor mwakani katika pambano lisilo la ubingwa.
Mabondia hao walipigana mwaka 2017 na Mayweather ambaye kwa sasa ana miaka 45 akaibuka mshindi na tangu astaafu ngumi amekuwa akishiriki mapambano yasiyo rasmi au yasiyo ya ubingwa na sasa anamtaka McGregor kwa mara nyingine.
“Hatujui kama litakuwa pambano rasmi, lakini mimi ningependa iwe pambano lisilo rasmi,” alisema Mayweather huku akitaka pambano hilo lipiganwe katika Uwanja wa Allegiant, Las Vegas.
“Tayari wameshazungumza na mimi kuhusu kile nitakachopata, unajua tutaanza na japo milioni 100 kwa Floyd Mayweather,” alisema bondia huyo ambaye pia anajiandaa kwa pambano jingine lisilo rasmi nchini Japan wikiendi hii dhidi ya Mikuru Asakura.
Mayweather ambaye amestafau ngumi akiwa na rekodi ya mapambano 50 bila kupigwa hata moja, amekuwa akishiriki mapambano kadhaa ya maonyesho au yasiyo rasmi ikiwamo lile la mwaka jana dhidi ya Logan Paul.
Kwa upande wake, McGregor alirudi katika ubingwa wa UFC baada ya kupoteza pambano lake dhidi ya Mayweather lakini tangu hapo amekuwa akihaha kurudi katika ubora wake uliomfanya awe bingwa mara mbili wa UFC na katika mapambano yake manne ya UFC ameshindwa mara tatu
McGregor mwenye umri wa miaka 34 hata hivyo kwa sasa anauguza majeraha ya mguu baada ya kuumia mwaka jana katika pambano lake dhidi ya Dustin Poirier ambalo pia alipoteza.
Ngumi Mayweather amtaka McGregor ulingoni
Mayweather amtaka McGregor ulingoni
Green SportsAuthor / Greensports Media LTD
Greensports author
Read also
