Na mwandishi wetu
Kocha wa muda wa Simba Juma Mgunda, ameeleza kuwa ushindi walioupata jana dhidi ya Tanzania Prisons ulitokana na juhudi na upambanaji wa wachezaji wake licha ya uchovu waliokuwa nao kutokana na kukosa muda mzuri wa kupumzika.
Katika mchezo huo wa Ligi Kuu ya NBC uliopigwa kwenye Uwanja wa Sokoine, Mbeya, Simba iliibuka na ushindi wa bao 1-0 na kufikisha pointi 10 ambazo ziliwapaisha kwenye msimamo wa ligi hiyo.
“Tangu huko nyuma historia inaonyesha mechi ya Simba na Prisons ni ngumu na imedhihirisha tulipambana kwa muda wote wa mchezo tukabadilisha hadi mfumo lakini wenzetu walikuwa vizuri kutuzuia na kufanya mashambulizi ya kushtukiza hadi walipofanya kosa tukalitumia vizuri dakika za mwisho,” aisema Mgunda.
Mgunda alieleza kuwa ushindi huo una maana kubwa kwao, kwanza kuendelea kujiweka katika nafasi nzuri kwenye msimamo na pili umewapunguzia wachezaji presha na kuwapa ari ya kupambana zaidi katika mechi zijazo za ligi na mashindano mengine.
Kocha huyo pia aliwapongeza Prisons kwa kuonyesha ushindani wa kweli kwenye mchezo huo ambao waliutumia kama maandalizi ya mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Nyasa Big Bullets ya Malawi utakaopigwa Uwanja wa Mkapa, Jumamosi ya keshokutwa.
Soka Mgunda: Upambanaji umetuokoa kwa Prisons
Mgunda: Upambanaji umetuokoa kwa Prisons
Green SportsAuthor / Greensports Media LTD
Greensports author
Read also
